Rayvanny Ft Zuchu – Number One Lyrics

Download mp3

Play Audio

Number One Lyrics – Rayvanny Ft Zuchu

Macho yalikuona, moyo ukakuchagua
Mdomo ukasema nakupenda aah
Mwambie umepona alokutesa moyo kuusumbua
Maumivu yamekwenda

Mi ni zawadi nilopewa
Macho nipepese wapi
Mi kipofu kwako sioni
Penzi limetaratadi, napepewa
Harufu ya marashirashi
Nikitouch touch shingoni

Uvae baibui khanga
Viatu vya kuchuchumia kangaroo
Kisima tui tanga
We huba nifukizia pambe tu

Ukizungushia shanga
Inashuka inapanda chini juu
Nishatafuna karanga
Sasa chumba ndo kiwanda watoto tu iyee iyee

Number one, you’re my number one
Number one, you’re my only one
Number one, you’re my number one
Number one, you’re my only one

Lalala, la la la
La- la-la mmmh

Hausukumi damu moyo
Unasukuma upendo wangu
Niko mahabani mambo sawa
Sawaa…

Penzi nalimung’unya kibogoyo
Nimepata size yangu
Yaani nalioga sio kunawa
Nawaa…

Filimbi nitapuliza
Kuita ndege waje
Raha zimefululiza
Kwako natokaje?

Hadi Bububu umepitiliza
Tuko kwa bibi Paje
Taratibu unaniliza baba

Tulivuruge varanga
Chimeneza kunengua kwangaru
Nikiandae kitanda
Shuka za maua ua ya marooon

Kisha tugonge na venta
Mambo ya kujizimua na varu
Nifunge upande khanga
Babu Juma we kwarua kwa kwaru

Ooh baby you are my…
Number one, you’re my number one
(My one and only)
Number one, you’re my only one

Baby my (number one)
Baby my (you’re my number one)
Aiaah oooh oooh
Number one, you’re my only one

Penzi limetaratadi, napepewa
Harufu ya marashirashi
Nikitouch touch shingoni

Rayvanny Ft Zuchu – Number One Lyrics

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *